У нас вы можете посмотреть бесплатно LORI LAANGUSHA MIFUKO ILIYOBEBA KEMIKALI 'AINA YA SULPHUR', ASKARI WALIFIKA ENEO HUSIKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Pwani, limefanikiwa kuondoa sumu (kemikali aina ya sulphur) iliyokuwa imemwagika barabarani eneo la Chalinze baada ya lori kuangusha mifuko iliyokuwa imebeba sulphur hiyo na Wananchi wakaanza kusogelea ili waichote. Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Pwani Jenifa Shirima amesema “Leo asubuhi tulipokea taarifa ya kemikali kumwagika Chalinze, Askari walifika na kukuta kemikali aina ya sulphur ikisafirishwa kuelekea Nchi jirani, hatua ya kwanza ilikuwa kutoa elimu kwa Wananchi kwani wengine walionekana kutaka kuchota kemikali ile na wakashirikiana na Trafiki kuruhusu magari kupita upande mmoja ambao haukuwa na kemikali” “Ikumbukwe sulphur inaweza kuleta madhara kiafya kwa Binadamu ikivutwa au kugusana na mwili wa Binadamu lakini pia penye msuguano inaweza kusababisha moto, kwahiyo hatua zote za tahadhari zilichukuliwa na tulisafisha eneo lile na kuizoa kemikali ile na kuruhusu magari kupita” “Rai yangu kwa Wananchi wanapoona kemikali hatarishi au chochote kimemwagika wasiwe wepesi kukimbilia kwani wanaweza kupata madhara, wanatakiwa kusogea mbali na kupiga simu 114 ya Jeshi la Zimamoto ili tufike kutoa msaada wa dharura, kwa Wasafirishaji natoa rai wanaposafirisha kemikali waziweke kwenye kontena ambazo ni salama na wazingatie maelekezo ya Mamlaka zinazowapa vibali kuhusu namna ya kusafirisha kemikali hizo”