У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WA MBWENI ZANZIBAR WAIBUKA TENA KUPINGA UWEPO WA BAA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ZANZIBAR Wananchi wa eneo la Mbweni, Zanzibar, wameeleza kupinga vikali uwepo wa baa na kumbi za starehe katika maeneo yao ya makazi, wakidai kuwa hali hiyo imekuwa chanzo cha kuporomoka kwa maadili na kuongezeka kwa vitendo vya kihalifu katika jamii. Kauli hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti wakati wa muendelezo wa kikao cha wananchi kilicholenga kujadili kadhia hiyo na kutafuta suluhisho la kudumu kwa manufaa ya wakazi wa eneo hilo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao walitaja matukio mbalimbali yanayodaiwa kujitokeza mara kwa mara, ikiwemo vurugu, wizi na vitendo vya kihuni. Aidha, walieleza wasiwasi wao juu ya baadhi ya watu wanaodaiwa kutumia magari kufanya vitendo vya ngono katika maeneo ya makazi, hali wanayosema inachafua maadili na kuathiri malezi ya watoto. Akizungumzia maazimio ya kikao hicho, Dkt. Saada Mkuya, ambaye ni mmoja wa viongozi wa kamati ya wananchi wanaopinga uwepo wa baa hizo, amesema hatua inayofuata ni kuandika barua rasmi kwa mamlaka husika ili kuwasilisha pingamizi lao pamoja na kueleza athari zinazotokana na uwepo wa baa na kumbi za starehe katika eneo lao. Amesisitiza kuwa lengo la wananchi si kupinga maendeleo, bali ni kulinda ustawi wa jamii, maadili na usalama wa watoto na familia kwa ujumla. Wananchi hao wameziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua za haraka ili kurejesha utulivu na maadili katika eneo hilo.