У нас вы можете посмотреть бесплатно Vurugu, Highlights & Interviews: Mbeya City 1-1 Yanga SC (VPL – 22/4/2018) или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC, wakicheza ugenini kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, wametoka sare ya bao 1-1 na wenyeji wao Mbeya City katika mchezo wa ligi hiyo uliopigwa jioni ya leo. Nyota wa zamani wa Mbeya City, Raphael Daud ndiye aliyewaadhibu waajiri wake hao wa zamani akifunga bao la kuongoza kwa Yanga dakika ya 58 akimalizia mpira wa adhabu ndogo aliotengewa na Juma Abdul. Katika mchezo huo wa 25 kwa Mbeya City na 23 kwa Yanga, Mbeya City walisawazisha bao hilo kupitia kwa Idd Suleiman aliyeingia kipindi cha pili, akifunga bao hilo dakika ya kwanza kati ya sita za nyongeza baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo, akimalizia pasi iliyotoka kwa Kenny Kunambi. KADI NYEKUNDU Hata hivyo Mbeya City ililazimika kuchezo pungufu kwa zaidi ya dakika 25 baada ya beki wake Ramadhan Malima kutolewa nje kwa kadi nyekundu, ikiwa ni kadi ya pili ya njano kwa kuonesha mchezo usio wa kiungwana. VURUGU Mchezo huo ulikumbwa na vurugu na kulazimika kusimama kwa takriban dakika 5. Vurugu hizo zilihusisha mashabiki walioonekana kutoridhishwa na maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo, huku baadhi yao wakirusha mawe uwanjani, hali iliyotulizwa na askari, kisha mchezo kuendelea. WACHEZAJI WA MBEYA CITY KUZIDI Mbali na vurugu hizo, mchezo huo pia umekumbwa na utata katika dakika za nyongeza ambapo makocha wa Yanga hasa Shadrack Nsajigwa, ameonekana akilalamika kuwa wachezaji wa Mbeya City walikuwa 10 uwanjani badala ya 9 waliostahili kutokana na mmoja wao kuwa nje kwa kadi nyekundu.