У нас вы можете посмотреть бесплатно DKT. AKWILAPO AZUNGUMZA NA WATUMISHI HALMASHAURI YA MJI MASASI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
“𝐖𝐀𝐓𝐔𝐌𝐈𝐒𝐇𝐈 𝐓𝐔𝐏𝐄𝐋𝐄𝐊𝐄 𝐓𝐀𝐁𝐀𝐒𝐀𝐌𝐔 𝐊𝐖𝐀 𝐖𝐀𝐍𝐀𝐍𝐂𝐇𝐈 𝐊𝐖𝐀 𝐊𝐔𝐓𝐎𝐀 𝐇𝐔𝐃𝐔𝐌𝐀 𝐁𝐎𝐑𝐀” 𝐌𝐇𝐄. 𝐃𝐊𝐓. 𝐀𝐊𝐖𝐈𝐋𝐀𝐏𝐎 Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Masasi Mjini Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo amewaasa watumishi wa umma kuhakikisha wanapeleka tabasamu kwa wananchi kwa kutoa huduma bora na zinazostahili katika maeneo yao ya utumishi. Amesema hayo Desemba 23, 2025 wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Masasi katika kikao cha kwanza na watumishi kilichofanyika katika Ukumbi wa Jengo la Utawala. Amebainisha mambo matano muhimu ya kuyafanyia kazi kwa kina ikiwemo Kuwawezesha wananchi kuongeza kipato, kuboresha maisha ya watu na ustawi wa jamii (afya, elimu, maji,umeme, utawala bora), Kuimarisha miundombinu ya kisasa ya usafiri na usafirishaji na Halmashauri kufungua njia, Kudumisha utawala bora kwa kufanya kazi kwa utu( kazi na utu) na Kulinda na kuimarisha amani na usalama wa Nchi kwani ulinzi unamtegemea kila mwananchi. “Watumishi tunajukumu kubwa na la msingi la kupeleka tabasamu kwa wananchi kwa kutoa huduma bora, tuna mambo matano makubwa ambayo nimeyasema hapa ikiwemo kuboresha elimu, afya, upatikanaji wa maji, tuondoe kero za umeme, kuongeza kipato kwa wananchi, wafanyabiashara wafanye kazi vizuri na mengine mengi na yote haya yanawezekana tukiendelea kuimarisha ulinzi, usalama na amani katika Nchi ” amesema. Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Masasi Mhe. Sospeter Nachunga amesema Halmashauri imejipanga vyema katika kuongeza mapato ya ndani ya Halmashauri huku akifikisha salamu za pongezi kwa Mbunge kutoka kwa watumishi na kwamba wanakwenda kutekeleza maelekezo ya viongozi na kuyafanyia kazi kwa kuzingatia taratibu, kanuni, sheria na miongozo mbalimbali ya Serikali.