У нас вы можете посмотреть бесплатно Mafunzo ya Ushonaji, Ubunifu wa Mavazi na Teknolojia ya Nguo yanayotolewa VETA Dakawa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mpenzi mtazamaji Ushonaji na Ubunifu wa mavazi ni miongoni mwa sekta ambazo hivi karibuni zimeonyesha mchango mkubwa katika maendeleo ya viwanda nchini. Sekta hii imezalisha ajira kwa vijana wengi hasa ajira binafsi na hivyo kuwawezesha vijana hao kutengeneza kipato kwa ajili ya kuendesha maisha yao na jamii kwa ujumla. Viwanda vya uzalishaji nguo, navyo vimekuwa vikihitaji nguvu kazi yenye ujuzi wa kutosha katika kuendesha viwanda hivyo huku msisitizo ukiwa ni kuzalisha nguo zenye ubora unaokubalika kimataifa na kupunguza utegemezi wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi. Msisitizo wa Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha viwanda vingi zaidi vinaanzishwa ili kuwezesha ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. Uanzishwaji wa viwanda vya nguo nchini, unazaa mahitaji ya nguvu kazi bora ya kutosha yenye stadi stahiki za kuwezesha uzalishaji wa nguo zenye ubora hapa nchini. VETA imekuwa ikitoa stadi na kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi wa kutosha katika kuwezesha uzalishaji na ubunifu wa mavazi bora. katika kipindi hiki tumeangazia kwa kina mafunzo ya ushonaji na teknolojia ya mavazi ambapo tutaweza kujionea namna mafunzo hayo yanavyotolewa katika hatua mbalimbali katika chuo cha VETA Dakawa.