У нас вы можете посмотреть бесплатно USIPASUKE MOYO, MWAMBIE YESU. WAFILIPI 4:6-7 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Utangulizi Dunia imejaa mambo yanayosumbua mioyo yetu. Mengine yanatupa kuwaza sana (mfano: hali ngumu ya maisha); mengine yanatupa wasiwasi (mfano: taarifa za wasomi kuhusu uwezekano wa kudorora kwa uchumi, na mambo yaliyo nje ya uwezo wetu na ambayo hatujui yatatokeaje au yataishaje); mengine yanatupa woga (mfano: taarifa mbaya kutoka kwa madaktari kuhusu afya yako na mambo mengine yanayotisha); mengine yanatukwaza; mengine yanaleta uchungu na maumivu moyoni (mfano: tunapoonewa, tunapodhulumiwa, tunapoona haki haijatendeka, tunapopoteza mali na/au tunapopoteza wapendwa wetu); n.k Mambo ambayo Mungu anataka tufanye 1. Sala (prayer): haya ni maombi ya jumla na yenye mwongozo unaojulikana. Mfano mzuri ni Sala ya Bwana (Mathayo.6:9-13). Unapokutana na mambo yanayosumbua moyo, sehemu ya kuanzia ni kwenye Sala ya Bwana. 2. Maombi (supplication/petition2): haya ni maombi ya kina, yanayogusa maeneo mahsusi na yanafanyika kulingana na uhitaji uliopo na uongozi wa Roho Mtakatifu kwa wakati huo. Maombi haya ni kama wakili anavyokwenda mahakamani kuwasilisha hoja zake. Isaya 41:21 3. Kushukuru (thanksgiving): inahusisha kumshukuru Mungu kwa yale ambayo ameshatenda na kwa yale ambayo tunaamini atatenda. Hata katika nyakati ngumu na za sintofahamu, bado Mungu anasisitiza kwamba tumshukuru. NB: Jambo la muhimu ni kuhakikisha kwamba haja zetu zinajulikana na Mungu. Tukishafanya hilo, hatutakiwi tena kusumbuka mioyo hata kama tunaona Mungu hajafanya kama tunavyotaka au kwa wakati tunaotaka. Tunatakiwa kujua kwamba sisi ni watoto wake na Yeye ni Baba yetu; hivyo, hatuna haja ya kusumbuka au kuteseka mioyo maana Yeye (Mungu) anajua namna bora ya kutupa haja zetu.