У нас вы можете посмотреть бесплатно Profesa Kabudi awashukia wanaobananga Kiswahili, aitaka Serikali kuchukua hatua или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mbunge wa Kilosa, Profesa Palamagamba Kabudi amesema licha ya Tanzania kuwa kinara wa lugha ya Kiswaili ila tusijidanganye kuwa ndio pekee wenye Kiswahili sanifu na fasaha, bali zipo pia Kenya, Congo, Burundi na Rwanda ambako kuna wazungumzaji wa lugha hiyo. Amesema ili kubaki kuwa kinara, inabidi kushughulikia vihatarishi vitatu ambavyo vimeanza kujitokeza na visipofanyiwa kazi tutaporomoka katika umaarufu. “Imezuka hulka sijui imetoka wapi ya kudondosha ‘h’, huyo amekuwa uyu, huyo amekuwa uyo kwa miaka mingi tatizo hili limekuwa la kotana ya Kaskazini Magharibi ya Tanzania, lakini limehama na kutamalaki Tanzania nzima.” Profesa Kabudi ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kutumia vyombo vya habari redio za kijamii na TV kusahihisha ubanangaji wa lugha, pia ametaja kihatarishi kinginge ni mtindo wa kufubaza Kiswahili. “Maneno mengi ya matumizi ya kawaida kwa sababu ya kufikiria ngono ngono tumeyapa maana isiyo yenyewe na matokeo yake tumeyaondoa katika matumizi ya kawaida, badala ya matiti tunasema nyonyo, toka lini teno matiti lilikuwa baya, lakini kwa sababu tunafikiri visivyofikirika tunaanza kuondoa maneno ya Kiswahili na kukifubaza.” Kabudi ameyasema hayo leo Mei 23, 2024 wakati akichangia mjadala bungeni wa kupitisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2024/2025, jijini Dodoma.