У нас вы можете посмотреть бесплатно Askofu Sangu: Fanya utume wako kwa Upendo или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wakristo na watu wote wenye mapenzi mema wameaswa kumuomba Roho Mtakatifu ili awasaidie katika kutenda kazi ya kuhubiri na kutangaza Injili ya KRISTO. Wito huo umetolewa leo Julai 20, 2023 na Mhashamu Askofu LIBERATUS SANGU wa Jimbo Katoliki SHINYANGA kwenye homilia yake, aliyoitoa kwa waamini wakati wa Adhimisho la Sadaka ya Misa Takatifu ya utoaji wa Daraja Takatifu ya Upadre kwa aliyekuwa Shemasi SOSTHENES NTEMI CHARLES, kutoka Parokia ya Mtakatifu LUKA BARIADI Mkoa wa SIMIYU Jimbo Katoliki SHINYANGA. Askofu SANGU amesema kuwa ukimpokea Roho Matkatifu utampeleka kwa watu wengine kwa upendo, huku upendo huo ukianzia kwa familia, Jumuiya na jamii inayokuzunguka. Aidha, amewataka wakristo wanapompokea Roho Mtakatifu waishi na kumuonesha kwa vitendo kwa watu wanaowazunguka badala ya kuwa watu wa masengenyo na vitendo ambavyo havimpendezi MUNGU. Hata hivyo Askofu amemtaka Padre Mpya afanye utume wake kwa upendo, huku akimhubiri KRISTO, bila kuchoka na wala kukata tamaa, huku akiongozwa na Roho Mtakatifu. Vile vile, amemtaka Padre mpya kujibidiisha katika kufanya kazi yake ya utume aliyoitiwa na MUNGU kwa unyenyekevu, utii na upendo mkubwa huku akiongozwa na MUNGU mwenyewe. Askofu LIBERATUS SANGU amemshukuru MUNGU kwa utume wake ndani ya Jimbo Katoliki SHINYANGA ambapo toka azimikwe kuwa askofu wa Jimbo hilo, amewapadrisha mapadre 33 na kwa idadi hiyo imepeleka kufikia mapdre 78 ndani ya jimbo hilo. www.radiombiu.co.tz #RmSautiYaFaraja