У нас вы можете посмотреть бесплатно MWAKILISHI MAHONDA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA NA KUTUMIA VIZURI MRADI WA MAJI KITOPE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda, Ndugu Mboja Ramadhani Mshenga, amewataka wananchi wa Kijiji cha Kitope kutumia ipasavyo Mradi wa Maji ulioanzishwa katika kijiji hicho kwa lengo la kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu. Ameyasema hayo wakati wa hafla ya kukabidhi tenki la maji pamoja na shilingi laki tatu kwa ajili ya ukarabati na uboreshaji wa mfumo wa usambazaji wa maji kwa wananchi wa Mahonda, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesisitiza umuhimu wa wananchi kutumia maji hayo kwa nidhamu, kuzingatia usanifu wa mradi na kuondoa tofauti zozote katika upatikanaji na usambazaji wa huduma hiyo muhimu. Aidha, Mwakilishi huyo ameutaka uongozi wa Shule ya Msingi Kipandoni kutumia fedha zilizotolewa kutatua kero zinazowakabili wanafunzi, kwa lengo la kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuongeza upatikanaji wa elimu kwa haraka.