У нас вы можете посмотреть бесплатно MAELFU YA WANANCHI WA MKOA WA NJOMBE WAJITOKEZA KUMDHAMINI RAIS SAMIA KUWANIA URAIS KUPITIA CCM или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Njombe wamejitokeza kwa wingi kumdhamini Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwania nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Tukio hilo limefanyika kwa hamasa kubwa likishirikisha wananchi wa kada mbalimbali ndani ya CCM, wakiwemo vijana, wanawake na wazee, waliokuja kuonyesha mshikamano wao kwa uongozi wa Rais Samia. Wananchi hao wameeleza kuwa uongozi wa Rais Samia umeleta mabadiliko makubwa katika sekta za maendeleo ikiwemo elimu, afya, miundombinu na diplomasia, huku akisisitiza ushirikiano na mshikamano wa kitaifa. Wamesema miradi mikubwa inayoendelea nchini ni kielelezo cha dhamira yake ya dhati ya kuwaletea Watanzania maendeleo endelevu. Aidha, waliwataka Watanzania wote kuungana kwa mshikamano na kumuunga mkono Rais Samia katika safari ya kuendeleza Taifa, wakibainisha kuwa kumdhamini ni kuhakikisha kuwa mipango na miradi aliyoanzisha inakamilika kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.