У нас вы можете посмотреть бесплатно Mimba kuharibika kutokana na utofauti wa Damu ya Baba na Mama | Visababishi na Jinsi ya kuepuka!?? или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mimba kuharibika kutokana na utofauti wa magroup ya damu,Mimba kuharibika miezi mitatu ya katikati,Mimba kuharibika miezi mitatu ya mwishoni,Mimba kuharibika miezi mitatu ya mwanzoni,Mimba kuharibika kabla ya kujifungua na Dr.Mwanyika. Baadhi ya Akina Mama na Akina Dada bila kujua shida inayoweza kujitokeza baada ya kujifungua au kutoa Mimba endapo kama wao Damu zao zina Rh -Ve na walikutana na wanaume wenye Damu ambazo zina Rh +Ve kwa bahati mbaya Kijusi au Mtoto aliyeumbwa alikuwa na Rh +Ve kwa bahati mbaya zaidi wakati wa kujifungua au kutoa Mimba hiyo Damu ya mtoto ilichanganyika na Mama mwisho wa siku wao wenyewe hawakupewa Anti-D immunoglobulin na Miili yao ikaanza tengeneza anti -D alloantibody (Maternal Sensitization/Isoimmunization) A. Kwa yule Dada ambaye ametoa Mimba na amekuwa sensitized ina maana endapo akikutana na mwanaume mwenye Rh +Ve atapata mtoto kwa shida sana na anaweza kuwa kwenye hatari ya kupoteza Mimba au Watoto muda mchache Mara baada ya kujifungua! B. Kwa yule Mama ambaye amebahatika kujifungua mtoto wa kwanza salama na hakupewa ile anti -D immunoglobulin maana yake atapata shida sana kupata mtoto kwenye Mimba ya pili na kuendelea hii ni kwa sababu ya uharibifu wa seli nyekundu za Mtoto na kufanya mtoto afie tumboni mwa Mama au kujifungua mtoto mwenye upungufu wa Damu na kupoteza maisha yake. Kama Mama au Dada umepata Mimba nenda clinic mapema chini ya wiki 12 ili ukafahamu kundi la Damu yako na endapo kundi la Damu yako lina Rh -Ve utatakiwa umshirikishe Mumeo ambapo endapo Mume ana Rh +Ve, Mimba itakapofikisha wiki 28 na 34 mpaka 36 mama utatakiwa upewe Anti-D immunoglobulin na vile vile ufanyiwe kipimo ilikujua antibodi zimetengenezwa kiasi gani ili kuangalia hatari ya mwanao kuwa salama au lah! Mama au Dada kama una Rh -Ve utatakiwa kuchoma sindano ya Anti-D immunoglobulin kila utakapofanya Mambo haya hapa chini; 1. Kila Mimba inapoharibika au Endapo umetoa Mimba kwa njia haramu! (ndani ya masaa 72). 2. Kila Unapojifungua Mtoto wako! (Ndani ya masaa 72). 3. Kutokwa Damu kwa aina yoyote wakati wa Ujauzito ikihusisha kutokwa Damu Mimba ikifikisha wiki 28 {APH - PP & AP) 4. Mimba kutunga Nje ya Mfuko wa Uzazi. 5. Ajali inayohusisha tumbo na kutokwa damu, ECV na AC. Mambo yanayoweza kutokea endapo hujapewa Anti-D immunoglobulin na umekuwa sensitized. 1. Mimba kuharibika Mara kwa Mara. 2. Kujifungua mtoto ambaye anaweza kupoteza maisha mapema Mara baada ya kujifungua au kujifungua mtoto akiwa amefariki. 3. Kujifungua Mtoto mwenye upungufu wa Damu. 4. Kujifungua mtoto aliyejaa maji (Hydrop fetalis) na nk KUMBUKA; Uonapo Dalili hizo wakati wa Ujauzito basi unatakiwa kupata ushauri kutokwa kwa Mkunga au Daktari ili kuhakikisha unakuwa na Afya! NB: Ukitaka kujifunza zaidi ni fuatilie YouTube kwa jina la Dr.Mwanyika au bonyeza link hapo 👇👇👇👇 / drmwanyika Ukiwa unamaswali unaweza kuuliza hapa chini (kwenye comments za youtube). Subscribe,Comment and Share JapideAfya_Services Your Health is Our Health Instagram as @JapideAfya_Services Facebook page as @JapideAfya_Services ©Dr.Mwanyika. #MamaAfya #ShidaDamuni #JapideAfya_Services