У нас вы можете посмотреть бесплатно WAHITIMU 336 VETA MWANZA WAPEWA MCHONGO WA KAZI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WAHITIMU 336 VETA MWANZA WAPEWA MCHONGO WA KAZI Shirika lisilo la kiserikali la Plan International, kupitia mradi wake, wa elimu na makuzi kwa vijana,(VEMA) limewalipia ada vijana 336 katika Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mkoa wa Mwanza ili kujifunza mafunzo mbalimbali ya ujuzi katika chuo hicho cha ufundi. Akizungumza na vijana hao wahitimu, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Amri Mkalipa, amewataka vijana hao kuyatendea haki mafunzo waliyopatiwa ili waweze kujiajiri na kujipatia kipato kupitia ujuzi walioupata VETA. Kwa upande wake, Mratibu wa Mradi wa Plan International, Gabriel Kayanda, amesema mafunzo hayo yamegharimu kiasi cha shilingi milioni 100 kwa vijana 400, ingawa baadhi yao walishindwa kuendelea na mafunzo kutokana na sababu mbalimbali. Aidha, amesema shirika hilo limetoa vifaa kazi vikiwemo mashine za kuunganisha vyuma, vyombo vya kupikia, pamoja na vifaa vya ujenzi, ufundi bomba na umeme wa majumbani, vilivyogharimu zaidi ya shilingi milioni 65. Kwa upande wao, baadhi ya wahitimu, akiwemo Keven Danyeli na Estar Keny, wamesema kuwa kutokana na hali ngumu ya maisha, wanashukuru kupatiwa mafunzo hayo kwani yatawasaidia kujikwamua kiuchumi na kujitegemea