У нас вы можете посмотреть бесплатно MOTO WATEKETEZA MAGHALA YA KATANI MOROGORO, HASARA YAZIDI Sh700 MILIONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani Morogoro linaendelea kuchunguza chanzo cha moto ulioteketeza maghala ya Chama cha Ushirika wa Wakulima Morogoro (Mofacu), yanayotumiwa na Kampuni ya LMAX Limited kuhifadhi na kuchakata katani. Moto huo ulizuka usiku wa kuamkia leo, saa 6 usiku, karibu na kituo cha reli ya Kati katika Manispaa ya Morogoro. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Morogoro, Mkaguzi Ramadhani Khalid, akizungumza leo Jumatatu Machi 3, 2025, amethibitisha tukio hilo na kusema juhudi za kudhibiti moto zilifanikwa kwa kiasi kikubwa, huku uchunguzi wa chanzo cha moto ukiendelea. "Tumefanikiwa kuudhibiti moto na kuokoa maghala matatu pamoja na ofisi za kampuni hiyo. Hata hivyo, uchunguzi wa kina utafanyika ili kubaini chanzo cha moto huu," amesema Khalid. Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kampuni ya LMAX Limited, Evidius Rwegasira, moto huo umeharibu shehena kubwa ya katani pamoja na mitambo ya uchakataji, na kusababisha hasara inayokadiriwa kufikia zaidi ya Sh700 milioni.