У нас вы можете посмотреть бесплатно #SHUHUDIA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#UhamiajiUpDates Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini (CGI) Dkt. Anna Makakala leo jana tarehe 31 Machi 2022 katika Ofisi ya Uhamiaji Kurasini Jijini Dar es Salaam, Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan amemvisha cheo kipya na kumuapisha Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji (ACI) Hassan Ali Hassan aliyekuwa Afisa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Pemba na kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar. Mnamo tarehe 29 Machi, 2022 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan alimteua ACI Hassan Ali Hassan kuwa Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar na kumpandisha cheo ambapo leo rasmi amekula kiapo na kuvalishwa cheo kipya tayari kwa kazi. Baada ya Kuvishwa cheo kipya na kuapishwa Kamishna Hassan aliongozwa pia kutamka kiapo cha maadili ya utumishi wa umma na Katibu Msaidizi Kanda Maalumu Dar es Salaam kutoka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Bi. Elizabeth Komba. Kamishna Hassan Ali Hassan anachukua nafasi ya Kamishna wa Uhamiaji Johari Masoud Sururu ambae kwa mujibu wa taarifa ya mawasiliano Ikulu atapangiwa majukumu mengine. Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Makakala baada ya kumvalisha cheo kipya na kumuapisha amempongeza na kumtakia heri katika majuku hayo mapya na kumuahidi ushirikiano wa kutosha wakati wote ili kufikia dira na dhima ya Uhamiaji kwa manufaa ya Jeshi la Uhamiaji na Taifa kwa ujumla. Aidha amewataka maafisa na askari wengine kuendelea kuchapa kazi kwa Utii, Uhodari, Uaminifu na Weledi wa hali ya juu ili kufikia ndoto zao na si vinginevyo. Kwa upande wake Kamishna mpya wa Uhamiaji Zanzibar Hassan Ali Hassan amemshukuru rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini na kumteua katika nafasi hiyo. Kamishna Hassan ameeleza kwamba anaenda kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na weledi wa hali ya juu na kuahidi ushirikiano wa kutosha kwa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Tanzania ili kufikia dira ya Uhamiaji kuwa taasisi yenye ufanisi na inayotoa huduma za Uhamiaji zinazokidhi viwango vya kitaifa na kimataifa.