У нас вы можете посмотреть бесплатно SERIKALI YAKABIDHI BILIONI 7 KWA VIJANA 308 MRADI WA BBT UVUVI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekabidhi hundi ya shilingi Bil. 7 kuwezesha mitaji kwa vijana waliohitimu mafunzo ya program ya Jenga Kesho iliyo Bora kwa upande wa sekta ya Uvuvi (BBT-UVUVI) ambapo zitatumika kwenye shughuli za ukuzaji viumbe maji. Akizungumza kabla ya kukabidhi hundi hiyo Mgeni rasmi wa hafla hiyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Mhe. Joel Nanauka amesema kuwa fedha hizo zinatolewa kama mikopo yenye mashart nafuu kwa vijana kwa ajili ya kuwezesha mitaji, vifaa, pembejeo muhimu za ukuzaji viumbe maji pamoja na posho ya kujikimu kwa washiriki. "Program hii haitaishia tuu hapa , itaenda ukanda wa pwani na mtwara kwani mradi wenyewe una sura ya ukuzaji wa uchumi wa buluu ” Amesema Mhe. Nanauka Aidha amewakumbusha vijana wanufaika kuwa hii ni mikopo, wana wajibu wa kufanya marejesho kwa uaminifu ili fedha zinazopatikana ziweze kuwasaidia vijana wengine ambao wana uhitaji. Naye Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Ng'wasi Kamani amesema kuwa uwezeshaji wa vijana hao ni sehemu ya mikakati ya wizara ya kuongeza uzalishaji pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya uvuvi katika pato la Taifa sambamba na utoaji wa ajira nchini.