У нас вы можете посмотреть бесплатно #exclusive или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kama una ratiba za kunywa soda kila siku, hasa aina ya cola upo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa kisukari, Profesa Kaushik Ramaiya amesema. Amesema kwa kawaida binadamu anatakiwa kula vijiko vitano vya sukari kwa siku, ila baadhi ya vyakula vina sukari iliyozidi mfano soda yenye ujazo wa mil 350 ina sukari vijiko 10, juisi hali kadhalika. Kaushik ambaye ni daktari bingwa mbobezi wa magonjwa ya ndani na kisukari, amesema unywaji wa vinywaji vyenye sukari nyingi na mtindo wa maisha ni sababu ya ongezeko la wagonjwa wanaugua kisukari aina ya pili ‘Type 2 diabetes’. Wagonjwa wanaotibiwa kisukari wameongezeka katika kliniki nchini kutoka 464,110 mwaka 2019 mpaka kufikia watu 674,399 mwaka 2023 kwa mujibu wa takwimu za Mtuha za Wizara ya Afya. Akizungumza na Mwananchi katika mahojiano maalumu mapema wiki hii, amesema hali ya maisha inaweza kuchangia mtu kupata kisukari kwa zaidi ya asilimia 40 mpaka 50.