У нас вы можете посмотреть бесплатно CUF KWAZIDI KUFUKUTA, POLISI YAWATOA VIGOGO KIKAONI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mjumbe wa Baraza la Chama cha Wananchi (CUF), Mohammed Ngulangwa, pamoja na wenzake wawili, wamejikuta wakishikiliwa na Jeshi la Polisi na kutolewa nje ya kikao kinachoendelea cha baraza la chama hicho, ambacho kilikuwa kikijadili majina ya wagombea watakaoingia katika kinyang’anyiro cha nafasi za juu ndani ya chama. Sababu ya kuondolewa kwao katika kikao hicho, kilichogubikwa na kelele, makonzi na misukosuko ya hapa na pale, ni madai kwamba walikuwa wakipinga kila hoja iliyowasilishwa, jambo lililodaiwa kuwanyima wajumbe wengine utulivu. Kikao hicho kinaendelea katika makao makuu ya chama hicho, Buguruni, jijini Dar es Salaam. Ikumbukwe kuwa Ngulangwa na wenzake ni wafuasi wa Profesa Ibrahim Lipumba, na msimamo wao ni kwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa wa kutengua uchaguzi uliomweka madarakani uongozi mpya wa chama. Awali, Mwananchi ilizungumza na Ngulangwa na kumuuliza sababu za kushiriki kikao hicho ilhali msimamo wao haukubaliani na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa. Katika majibu yake alisema: “Huwezi kupinga jambo ukiwa nje ya mchakato. Naenda kushiriki ili niweze kupinga uamuzi utakaofikiwa,” amesema. Endelea kufuatilia Mwananchi