У нас вы можете посмотреть бесплатно Senator Mandago’s Family Still Seeks Justice After 7-Year Sentence или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Familia ya Seneta wa Uasin Gishu, Jackson Mandago, imesalia na majonzi baada ya Mahakama ya Eldoret kumhukumu Lemmy Kipkurui Kosgey kifungo cha miaka saba jela kuhusiana na kifo cha mwaka 2019 cha Johana Kirwa Kinyor, kaka mkubwa wa seneta huyo. Hakimu Mkuu Mwandamizi Peter Areri alimpata Kosgey na hatia ya wizi wa kutumia nguvu na kupatikana na mali ya wizi, kufuatia kupatikana kwake na simu ya marehemu muda mfupi baada ya tukio. Kinyor, aliyekuwa na umri wa miaka 56, alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Kenya Pipeline na alikuwa amehamishwa kutoka Kisumu kwenda Eldoret. Mwili wake ulipatikana Mei 2019 katika hoteli iliyokuwa ikiendelea kujengwa mjini Eldoret. Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, tukio hilo lilidaiwa kutokea kati ya Mei 25 na 26, 2019 katika Kituo cha Biashara cha Chepkanga, Kaunti ya Uasin Gishu. Licha ya uzito wa tuhuma za mauaji, mahakama haikutoa uamuzi wa moja kwa moja kuhusu nani aliyemuua marehemu, huku hukumu ikijikita katika makosa ya wizi na mali ya wizi. Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) iliwasilisha mashahidi watano, lakini kwa familia, swali kuu linasalia bila majibu: ni nani aliyemuua Johana Kirwa Kinyor?