У нас вы можете посмотреть бесплатно MWENYEKITI HALMASHAURI LUDEWA AONGOZA UGAWAJI WA MICHE 4,870 YA PARACHICHI MUNDINDI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
MWENYEKITI HALMASHAURI LUDEWA AONGOZA UGAWAJI WA MICHE 4,870 YA PARACHICHI MUNDINDI Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa na Diwani wa Kata ya Mundindi, Mhe. Wise Mgina, leo tarehe 2 Februari, 2026, ameongoza zoezi la ugawaji wa miche 4,870 ya parachichi kwa kaya 487 za Kijiji cha Mundindi, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuinua uchumi wa wananchi kupitia kilimo cha mazao ya biashara. Zoezi hilo lililofanyika katika kitalu cha Felisia Remijo Msamba, limewezesha kila kaya kukabidhiwa miche 10, chini ya uratibu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Akizungumza katika zoezi hilo, Mhe. Mgina amewahamasisha wananchi kupanda na kutunza miche hiyo ipasavyo, akibainisha kuwa zao la parachichi ni zao la muda mrefu lenye faida kubwa kiuchumi na linaweza kumuinua mkulima kwa kipindi kirefu cha maisha. Aidha, amesema Halmashauri itaendelea kuimarisha mikakati ya kuhamasisha kilimo cha mazao ya biashara kwa lengo la kuongeza kipato cha kaya na kuchochea maendeleo ya kiuchumi wilayani humo. Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Festo Mkomba, amempongeza Mhe. Mgina kwa uongozi wake na kuahidi kuendelea kutoa usaidizi wa kitaalamu kwa wakulima ili kuhakikisha miche inakua na kutoa mavuno bora. Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mundindi, Ndugu Stivin Mlelwa, ameishukuru Serikali kwa kuwapatia miche hiyo na kueleza kuwa kijiji kitaweka sheria ndogo za kuilinda ili iwe na manufaa ya muda mrefu kwa wananchi. Miche hiyo imepatikana kupitia ushirikiano kati ya Kijiji cha Mundindi na Shirika la COPRA, ambapo pande zote zimechangia gharama kwa asilimia 50 kwa 50.