У нас вы можете посмотреть бесплатно AFARIKI KWA AJALI TANGA AKIELEKEA MOSHI KWA KRISMASI,WANNE WAJERUHIWA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Tanga. Safari ya kusherehekea sikukuu ya Krismasi mjini Moshi imegeuka majonzi baada ya dereva wa gari dogo, Justine Jacobo Njau (32), kufariki dunia papo hapo na wengine wanne wakijeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea alfajiri ya Desemba 25, 2025, mkoani Tanga. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, ACP Almachius Mchunguzi, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 10:30 alfajiri katika Kijiji cha Taula, Wilaya ya Handeni, kwenye barabara kuu ya Chalinze kuelekea Segera. “Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linafanya uchunguzi wa ajali ya barabarani iliyotokea tarehe 25 Desemba 2025, majira ya saa 10:30 alfajiri, katika Kijiji cha Taula, Wilaya ya Handeni, kwenye barabara kuu ya Chalinze kuelekea Segera,” amesema Kamanda Mchunguzi. Amesema ajali hiyo ilihusisha gari dogo aina ya Toyota RunX lenye namba za usajili T.350 DZA lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Moshi na gari la mizigo aina ya Mitsubishi Fuso lenye namba za usajili T.857 DZK lililokuwa likitokea Segera kuelekea Chalinze.