У нас вы можете посмотреть бесплатно NENO LA SIKU | Mathayo 28 | Maombi Ya Kushinda Uzushi | Isaac Javan или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Leo tunamaliza kusoma kitabu cha Mathayo, na tunaenda kufanya maombi ya kushinda uzushi. Katika maisha tunayoishi, hakuna jambo baya kama kuzushiwa maneno ya uwongo na watu wakaamini. Kuna watu wamekata tamaa ya maisha kwa sababu ya kuzushiwa maneno ya uwongo. Kuna watu wamepoteza marafiki kwa sababu ya kuzushiwa maneno ya uwongo. Kuna watu wametengana na wapendwa wao kwa sababu ya uzushi. Kimsingi, uzushi ni kitu kinachoweza kuharibu maisha ya mtu. Lakini habari njema ni kwamba, YESU alishatuandalia majibu ya tatizo hili. Damu yake ilipomwagika, ilitufungulia njia ya kutembea katika ushindi ikiwa ni pamoja na kushinda roho za uzushi ziharibuzo. Katika maombi ya leo, tunaenda kuomba YESU atufungue na kutuweka huru. Mahali popote ambapo uliwahi kuzushiwa jambo baya la uwongo, siku ya leo YESU anaenda kukuponya na pia anaenda kukurudishia vyote ulivyopoteza na anaenda kukupa heshima katika maisha yako. Kwa hiyo utakapokuwa unaomba, nakutia moyo ufanye maombi kwa kumaanisha, na utauona mkono wa BWANA ukikupigania na kukushindia. Mwisho kabisa, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kuungana nami katika usomaji huu wa biblia pamoja na maombi. Asante kwa wote uliowashirikisha waungane nasi katika maombi haya. Hongera sana kwa kufanikisha kusoma neno la Mungu kutoka kitabu chote cha Mathayo. Nakutia moyo, endelea kurudia maombi tuliyokwishafanya, mpaka uone umepata matokeo mazuri. Baada ya siku saba tutaendelea na kitabu cha Marko. Mpaka hapo tutakapoonana tena, nakuacha na amani ya YESU. Damu ya YESU ikulinde na inene maneno mazuri kwa ajili yako. YESU akuonekanie na akuvushe katika mambo yako yote. YESU akupiganie na akutetee katika kila jambo linalogusa maisha yako. Neema ya KRISTO YESU isikupungukie. YESU akupiganie na akuweke panapo nafasi. Mungu Roho Mtakatifu akutie nguvu unapoendelea kurejea maombi tuliyokwisha fanya. Utunzwe na damu ya YESU tangu sasa na siku zote. Amen