У нас вы можете посмотреть бесплатно MTAA ALIOTEKWA POLEPOLE, MAJIRANI WASHANGAA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
BongoFive yafika Ununio, Mtaa wa Tanzanite na Rubi, kufuatilia taarifa za kutekwa kwa Humphrey Polepole BongoFive imewasili katika eneo la Ununio, Mtaa wa Tanzanite na Rubi, kufuatilia taarifa kuhusu madai ya kutekwa kwa Ndg. Humphrey Polepole, ambaye inadaiwa alikuwa akiishi katika moja ya nyumba zilizopo mtaani humo. Tukio hilo linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia leo. Kwa mujibu wa wakazi wa eneo hilo, mtaa huo huwa na utulivu mkubwa nyakati za mchana, na hata zaidi wakati wa usiku. Hata hivyo, baadhi ya majirani wamedai kuwa ni vigumu kufahamiana kwani kila mtu anaishi ndani ya geti lake binafsi, jambo linalofanya mawasiliano ya kijirani kuwa hafifu. Jirani mmoja, ambaye hakutaka kutajwa jina lake, amesema kuwa wana kundi la mawasiliano la mtaa huo (WhatsApp group), na taarifa kuhusu tukio hilo waliipata usiku. Aliyejitokeza kwenda eneo la tukio alieleza kuwa walipofika walihisi mtu alikuwa amevamiwa na watu wasiojulikana. Mwenye nyumba hiyo alipopigiwa simu alieleza kuwa hakuwa na taarifa kamili na aliahidi kumpigia mpangaji wake ili kufahamu ni nani aliyekuwamo ndani ya nyumba wakati wa tukio. Baadhi ya majirani wameeleza kushangazwa na tukio hilo, wakidai kuwa eneo hilo kwa kawaida ni salama. Wamesema kuna walinzi wa usiku wakiwemo Masai, ambao huangalia usalama wa mtaa huo, na hawafahamu kilichotokea usiku huo hadi taarifa zilipoanza kusambaa. Tunaendelea kufuatilia kwa karibu taarifa zaidi kuhusu tukio hili. Written by @yasiningitu