У нас вы можете посмотреть бесплатно MTOTO ALIYEGONGWA NA NYOKA AZIKWA MTWARA| FAMILIA YADAIWA 250,000| MKURUGENZI KAFUNDA AINGILIA KATI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Familia ya Mtoto aitwae Rajabu Saidi (12) aliyefariki dunia baada ya kung'atwa na Nyoka siku ya Juni 03, 2025 akiwa nyumbani kwao Kijiji cha Imekuwa kata ya Naumbu Halmashauri ya wilaya ya Mtwara, imeomba kupunguziwa au kusamehewa kiasi cha pesa wanachodaiwa katika Zahanati ya Kijiji hicho baada ya marehemu kupewa huduma ya kwanza ikiwa ni pamoja na sindano ya kuondoa sumu ya nyoka mwilini huku wakidai kuwa jumla ni Shilingi 250,000/= Akizungumza na Faida Online TV ilipofika katika Kijiji cha Msijute ambako ndiko ulikozikwa Mwili wa Marehemu, Mama aliyekuwa akimtunza Mtoto huyo aitwae Bi Habiba Litembe, amesema Mtoto huyo alikuwa anafukuza Mbuzi na ghafla akang'atwa na Nyoka, akakimbizwa kwenye zahanati ya Imekuwa ambapo baada ya kupata matibabu muda mchache baadae hali ya Mtoto huyo ilibadilika na kupewa rufaa kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula, lakini kabla hajafikishwa Ligula Mtoto huyo alifariki dunia. "Aliitwa mama mtu Chumbani, akanirejeshea mimi mrejesho kuwa kuitwa nilikoitwa mimi, tunadaiwa Shilingi 250,000/= kwa sindano ile ambayo ameitumia, baada ya hapo hali yake ikawa nzuri kidogo ila ghafla akabadilika" amesema Hamisi Ahmadi ambae ni Babu wa marehemu, mkazi wa Kijiji cha Majengo. Baadhi ya Viongozi wa Kata hiyo akiwemo Mwenyekiti wa Wazee kata ya Mayanga Mzee Saidi Hamisi Nawanda na Bi. Mwanaenzi Yusufu ambae ni Mwenyekiti wa UWT Kata hiyo ya Mayanga, wakiwa msibani hapo wameiomba Serikali kupunguza bei ya sindano hizo za kuondoa Sumu mwilini huku ukizingatia kuwa wengi wanaokumbwa na changamoto hizo ni Wananchi wa hali ya chini. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mtwara Bw. Abeid Abeid Kafunda, amesema kuwa zahanati zote zilizopo ndani ya Halmashauri hiyo zimesambaziwa Sindano hizo za kuondoa sumu mwilini, huku akiongeza kuwa Familia hiyo isamehewe kulipa kiasi hicho cha fedha wanachodaiwa, na yule atakaeng'atwa na Nyoka na kufariki ndani ya Halmashauri hiyo, basi Familia haitakiwi kulipa tena endapo itakuwa amepatiwa tiba ya sindano hiyo ya kuondoa sumu ya Nyoka mwilini. SUBSCRIBE YOUTUBE CHANNEL YA FAIDA ONLINE TV ILI KUPATA BAHARI ZETU HAKIKA SISI NI WATU WA FIELD