У нас вы можете посмотреть бесплатно RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI BARABARA KUU YA NJOMBE - MORONGA - MAKETE или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
RAIS SAMIA AFUNGUA RASMI BARABARA KUU YA NJOMBE - MORONGA - MAKETE Aelekeza Ujenzi wa Barabara ya Makete kuelekea Mbeya. Barabara ya Makete inafungua Fursa za uwekezaji, utalii na kuwezesha Wakulima kufikisha Mazao mjini. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Leo August 06 amezindua Barabara ya kiwango Cha Lami kutoka Njombe, Moronga mpaka Makete yenye urefu wa zaidi ya Kilomita 107.4 ambapo amesema kukamilika kwa Barabara hiyo kutachochea Kasi ya maendeleo Wilaya ya Makete. Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Barabara hiyo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi Mkoani Njombe, Rais Samia amesema Ujenzi wa Barabara hiyo umegharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 200 ambapo amewataka Wananchi kutunza na kulinda Miundombinu hiyo. Aidha Rais Samia amezitaja faida za Barabara hiyo kuwa ni pamoja na kuwezesha Wakulima kufikisha Mazao mjini na kupunguza adha ya kupanda kwa Bei ya mazao. Ili kuhakikisha kero ya Barabara kwa Wana Makete inakamilika, Rais Samia ameelekeza Wizara ya Ujenzi kuharakisha hatua za Ujenzi wa Barabara ya Makete kuelekea Mbeya ili kurahisisha usafirishaji. Pamoja na hayo Rais Samia ameelekeza Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na Halmashauri ya Makete kuweka utaratibu wa kuchangishana fedha kwaajili ya uwekaji wa Taa za Barabara ambapo amechangia Milioni 100 kwa Wizara na amesisitiza uchangishaji wa fedha kwa Wananchi na Wadau usiwe wa kero Bali kwa hiyari. Kwa upande wao baadhi ya Wakazi wa Makete akiwemo Mzee Reuben Tweve na Mzee Samwel Makutsu wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa Ujenzi huo na kubainisha kuwa tangu uhuru Wilaya hiyo haikuwahi kuwa na Barabara ya Lami. Katika uzinduzi huo Rais Samia pia amesikiliza kero na changamoto za Wananchi wa Makete ikiwemo ubovu wa Barabara ya Makete kuelekea Mbeya, punguzo la Bei ya pembejeo za kilimo, Bidhaa za Mafuta, Saruji na Sabuni ambapo zote zimetatuliwa papo kwa papo kupitia maelekezo kwa Mawaziri wa Wizara husika. SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA, TUJITOKEZE KUHESABIWA AUGUST 23