У нас вы можете посмотреть бесплатно MWILI WAKUTWA KWENYE DIMBWI LA MAJI KAHAMA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwili wa mwanaume mwenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka 25-30 ambaye hajafahamika jina wala makazi yake, umekutwa katika dimbwi la maji linalotumika kwa shughuli za bustani katika Mtaa wa Malunga, Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, mkoani Shinyanga. Tukio hilo limetokea leo Alhamisi, Julai 31, 2025. Shuhuda wa tukio, Maria Frank amesema aligundua uwepo wa mwili huo alipokwenda kuchota maji kwa matumizi ya nyumbani na kuona mtu akiwa amezama ndani ya dimbwi hilo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Janeth Magomi amethibitisha tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha kifo. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama. Kamanda Magomi pia amewataka wananchi kuhakikisha mashimo yenye hatari, ikiwemo madimbwi yanazibwa au kufukiwa ili kuepusha matukio ya aina hiyo. Video: Hellen Mdinda