У нас вы можете посмотреть бесплатно DCC MOSHI YABARIKI KUANZISHWA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA VUNJO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imepitisha kwa kauli moja mapendekezo mawili muhimu yaliyowasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndugu Shadrack Mhagama yakihusu uanzishwaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Vunjo pamoja na kupandishwa hadhi kwa barabara mbili za wilaya kuwa barabara za mkoa. Mapendekezo hayo yamekuja kufuatia ziara ya Dkt Mwigulu Lameck Nchemba, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliyefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi tarehe 20/02/2026. Mwongozo wa uanzishwaji wa mamlaka za serikali za mitaa ya mwaka 2014 umeainisha vigezo vya kisheria vinavyotakiwa kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mihtasari ya mikutano ya wananchi kutoka katika vijiji, kata, mamlaka ya mji mdogo pamoja na baraza la madiwani ikionyesha ridhaa ya wananchi kukubali kuanzishwa eneo jipya la utawala. Utekelezaji wa hatua za awali za maombi ya uanzishwaji wa Halmashauri ya wilaya ya Vunjo ulishafanyika ambapo mikutano ya vijiji 78, kata 14 (WDC) na kwa eneo la mamlaka ya mji mdogo mdogo wa Himo Vitongoji 18 na baraza 1 la mamlaka ilifanyika na wananchi 35,715 (WDC 220, Vijiji 33,995, na Vitongoji 1,501) walishiriki katika kutoa maoni yao na mihtasari iliwasilishwa katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi. Katika mikutano hiyo wanachi walioshiriki waliafiki kwa asilimia 100 ianzishwe Halamashauri ya Wilaya ya Vunjo, walieleza kuwa jambo ambalo wamelisubiri kwa muda mrefu maana wanatambua litasaidia kuwasogezea huduma karibu kama ilivyo malengo ya serikali.