У нас вы можете посмотреть бесплатно ROAD2RECOVERY; UAMUZI WA KUKOMBOA & KUMILIKI KILICHO CHAKO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
REV. DR. ADAMHAJJ asisitiza zaidi na kufafanua kwa undani ya kwamba kwa kila jambo au hoja kutimizwa linahitaji uamuzi.Twahitaji kupindua hali ya uchoyo, hali ya kuishi katika ubinafsi maishani mwetu. Hakuna kitakachobadilika katika ulimwengu wetu hadi pale kila mmoja wetu atakapokuwa radhi kubadilika. Mara nyingi huwa tunatamani ulimwengu ubadilike bila ya kukoma kutambua kwamba hali ilivyo ulimwenguni inatokana na njia tunazoishi katika maisha ya ubinafsi na chaguo tunalofanya kila siku. Ikiwa kila mmoja hapa duniani anafahamu jinsi ya kupokea na kuonyesha upendo, dunia yetu ingelikuwa mahali tofauti kabisa pa kuishi. Nafikiri sote twafahamu kuwa kuna jambo lililo kasoro katika jamii na kwamba lahitaji kutatuliwa. Lakini hakuna mtu anayefahamu kinachopaswa kufanywa au jinsi ya kuanza kufanya mabadiliko. Jibu letu kwa ulimwengu usioweza kuthibitika ni kulalamika na kufikiri, kuna mtu anayepaswa kufanya jambo fulani. Tunafikiri na kusema kuwa pengine Mungu au serikali au mtu mwingine yeyote aliye kwenye mamlaka anahitajika kufanya kitendo. Lakini ukweli ni kwamba kila mmoja wetu anahitajika kufanya jambo fulani. Lazima tujifunze kuishi maisha yenye mwelekeo tofauti kabisa na tulivyo sasa. Lazima tuwe radhi kujifunza, kubadilika na kukubali kwamba sisi ni sehemu ya tatizo lililoko. Hatuwezi kutatua kile tusichoelewa, kwa hiyo hitaji letu la kwanza ni kutafuta chanzo cha tatizo lililoko. Ni kwanini watu wengi hawana furaha? Ni kwanini ghasia zimeongezeka sana katika familia, maeneo jirani, miji na mataifa? REV. DR. ADAMHAJJ MINISTRIES For Support & Tithe : +254700146495 WATSUP : +254777700486