У нас вы можете посмотреть бесплатно Muhtasari wa matukio kwenye ziara ya Makamo wa Kwanza wa Rais majumbani Kaskazini Unguja или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, amesema kuna changamoto nyingi kwa familia duni, zinazohitaji mashirikiano kati ya viongozi na jamii, ili kuweza kuzikabili, hasa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Mheshimiwa Othman ameyasema hayo leo katika Ziara yake maalum ya kuwafariji na kuwapa pole wagonjwa, watu wasiojiweza na familia za wafiwa mbali mbali, ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema kuwa zipo changamoto ambazo siyo shida kuzitatua, bali baadhi yao zinahitaji mashirikiano ya pamoja kukabiliana nazo, kutokana na jinsi zinavyozorotesha na kudhoofisha ustawi wa watu, familia na jamii kwa ujumla, hali ambayo inagusa hisia za kila mwenye huruma. Mheshimiwa Othman ametolea mifano hali za unyonge, ufukara wa kupindukia, kuondokewa, maradhi, udhaifu na ukosefu wa kudumu wa kipato na mahitaji ya lazima, kuwa kwa sasa ni miongoni mwa changamoto zinazodhoofisha ustawi wa familia nyingi, katika visiwa vya Unguja na Pemba. Mheshimiwa Othman ametoa wito kwa jamii kuutumia vyema Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na kuhakikisha kunakuwepo mashirikiano ya kuwasaidia wale wasiojiweza wakiwemo wazee, wagonjwa, wajane, watoto yatima na watu wenye ulemavu, ili kutoa unafuu wa kupata huduma za msingi na ah-weni ya kimaisha. Wakiongelea juu ya wajibu wa kuwafikia na kuwasaidia watu wenye mahitaji na wasiojiweza, hasa katika Msimu huu wa Funga, Bw. Mohamed Nyasa Juma wa Donge-Njia ya Mtoni, na Bi Tatu Haji wa Bumbwini-Uwandani, pamoja na kushukuru juhudi za viongozi katika kufanikisha utoaji wa huduma na misaada kwa wananchi, wamesema wahitaji ni wengi, na wapo miongoni mwa watu hali zao ni dhaifu mno na za kukatisha tamaa, na hivyo kunahitajika kasi zaidi ya kuwakirimu. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Othman ametembelea pia Vijiji vya Kitope-Mkaratini, Kikobweni, Chutama, Muwange, Tazari, Mkokotoni, Mwanakombo na Langoni ambavyo ni katika Majimbo ya Mahonda, Nungwi, Chaani, Mkwajuni, Kijini, Tumbatu, Donge na Bumbwini, ndani ya Mkoa wa Kaskazini Unguja. Viongozi mbali mbali wa Serikali, Jamii, Vyama vya Siasa, na Vikosi vya Ulinzi na Usalama wamejumuika katika ziara hiyo wakiwemo Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo Zanzibar, Bw. Salim Bimani na Naibu Katibu wa Haki za Binadamu wa Chama hicho, Bi Pavu Juma Abdalla.