У нас вы можете посмотреть бесплатно DC TANGANYIKA AFURAHISHWA NA UWEKEZAJI WA MKULIMA KAKOSO, TANGANYIKA YAVUKA LENGO UPANDAJI MITI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi leo januari 30,2023 imeendelea na zoezi la upandaji miti ambapo mkuu wa wilaya ya Tanganyika Onesmo Buswelu amewaongoza Wakuu wa Idara mbalimbali na baadhi ya wananchi kupanda miti katika nyumba za Watumishi zilizopo eneo la Majalila. Miti hiyo imepandwa pembezoni mwa Barabara ya Polisi kuelekea mtaa wa nyumba za Watumishi. Mkuu wa wilaya Onesmo Buswelu amesema jumla ya miti 350 imependwa leo eneo hilo na kufanya jumla ya miti iliyopandwa katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika hadi sasa kufika Miloni 214,750 na kuifanya halmashauri hiyo kuvuka lengo la kitaifa linaloitaka kila halmashauri kupanda miti isiyopungua Milioni 1.5 Aidha, amewaonya wenye mifugo kulisha kwenye miche iliyopandwa na mazao ya wakulima pamoja na Wananchi wanaong'oa na kuiba miche iliyopandwa kuacha tabia hiyo mara moja. Nae Meneja TFS Wilaya ya Tanganyika Saimon Peter amesema zoezi hilo ni endelevu katika maeneo mbalimbali ya halmashauri hiyo licha ya kuwa wameshavuka lengo kwani miti bado ipo kwenye vitalu na watahakikisha inasambazwa kwenye Taasisi mbalimbali ili ipandwe. Katika hatua nyingine, DC Buswelu amemtembelea mkulima wa Mahindi, Karanga, Alizeti, Pamba na Tumbaku Bw. Abdalah Kakoso na kushuhudia uwekezaji mkubwa uliofanywa na mkulima huyo, hii ikiwa ni ukaguzi wa jitihada za Serikali baada ya kutoa mbolea ya ruzuku kama imefanyiwa kazi sawa na malengo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwakwamua wakulima. DC Buswelu amempongeza mkulima huyo na kutoa wito kwa maafisa Kilimo kuendelea kutoa ushauri kwa wakulima ili Kilimo chao kiwe na tija. Kwa upande wake Abdalah Kakoso ameishukuru Serikali kwa kuwawezesha wakulima kupata mbolea ya ruzuku tofauti na mwanzo ilivyokuwa inauzwa kwa bei holela hali iliyowafanya washindwe kupanua kilimo chao. Pia ameishukuru Serikali ya Tanganyika kwa kuwa karibu na wakulima hasa kitendo cha Mkuu wa wilya kumtembelea kimpempa nguvu na kuahidi kufuata maelekezo na ushauri anaopewa.