У нас вы можете посмотреть бесплатно ASKOFU KKKT AONYA BIASHARA YA CHUMVI NA MAFUTA NDANI YA NYUMBA ZA IBADA-ASKOFU-DKT MOLLEL или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
ASKOFU MOLLEL ATAKA VIONGOZI WA KANISA KUFUNDISHA KWELI YA MUNGU KWA JAMII Na James Stanley, Arusha – Tanzania Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dkt. Godson Mollel, amewataka viongozi wa kanisa kufundisha kweli ya Mungu kwa uaminifu bila kuyumbishwa na misukumo ya dunia ya sasa, akisisitiza kuwa mafundisho sahihi ni msingi wa kujenga washarika imara kiimani na kimaadili katika kipindi cha mabadiliko ya kijamii. Akizungumza katika ibada ya kuwabariki watheolojia kumi kuwa wachungaji iliyofanyika Usharika wa Iliboru, Jimbo la Arusha Magharibi, Askofu Mollel amewahimiza watumishi hao wapya kulitumikia kanisa kwa unyenyekevu, uadilifu na moyo wa kujitoa huku wakitanguliza kumtangaza Kristo na kuhudumia jamii bila ubaguzi. Ameongeza kuwa umoja wa kanisa, kusimama katika neno la Mungu na ushirikiano wa Wakristo ni nguzo muhimu ya kulinda maadili ya kiroho na kuimarisha huduma ya kichungaji kwa manufaa ya jamii. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Dayosisi hiyo, Mwalimu Loshillu Sambweti, amesema wachungaji wapya wanapaswa kuhubiri injili ya kweli kwa uaminifu, kuongoza washarika kwa mfano wa maisha yenye maadili mema na kusimamia huduma za kichungaji kwa bidii ili kuimarisha ukuaji wa kiroho na mshikamano wa kanisa. Baadhi ya wachungaji waliobarikiwa wamesema wamepokea wito huo kwa unyenyekevu na hofu ya Mungu, wakiahidi kulitumikia kanisa kwa uaminifu na kujitoa kikamilifu kwa washarika pamoja na kuendeleza mafundisho sahihi ya neno la Mungu.