У нас вы можете посмотреть бесплатно "UKEKETAJI NI KINYUME NA MPANGO WA MUNGU" или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dokta Dorothy Gwajima amelaani Vikali Vitendo vya Ukeketaji vinavyofanywa na jamii za wafugaji nchini, akisisitiza kuwa hakuna sababu za msingi zinahalalisha Vitendo hivyo katika jamii. Akizungumza mara baada ya kutembelea nyumba Salama ya Shirika "HIMD" Mkoani Arusha Dokta Gwajima Wamewataka wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu wanaofanya vitendo vya ukeketaji, wakidai kuwa nyama inayokatwa katika sehemu za siri za mwanamke wakati akikeketwa inasaidia katika uvuvi na Uchimbaji wa Madini. Hatua hiyo imekuja Baada ya wadau waliohudhuria sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Ukeketaji ambayo imeadhimishwa katika Shirika la "HIMD" kumweleza Waziri Dokta Gwajima juu ya Sababu iliyojificha nyuma ya vitendo vya ukeketaji ambayo ni Imani za kishirikina kuhusu Kuuzwa kwa viungo vinakatwa kwa wanawake wakati wa ukeketaji, kwamba vinasaidia kwenye uvuvi na Madini. Baadhi ya Waarithika wa vitendo vya ukeketaji wameiambia Radio Maria Tanzania kwamba ndoa za utotoni na Ukeketaji vimepoteza ndoto za Mabinti wengi waliopo katika jamii za wafugaji, huku Wakilishukuru Shirika la "HIMD" kwa kufufua matumaini yao baada ya kuamua kuwalea na kuwasomesha .www.radiomaria.co.tz #Miaka30yaradiomariaTz #Uinjilishajiupendonafaraja