У нас вы можете посмотреть бесплатно RC BABU AKEMEA UCHELEWESHAJI MIKOPO YA VIKUNDI MOSHI, ATAKA SH900 MILIONI IREJESHWE HARAKA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Moshi. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, amesema ucheleweshaji wa urejeshaji wa mikopo inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu umekuwa kikwazo kwa wananchi wengine wanaohitaji kunufaika na mikopo hiyo, akisisitiza kuwa wanufaika wote wanapaswa kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwezesha mzunguko wa fedha kwa makundi mengine. RC Babu ametoa kauli hiyo leo wakati wa hafla ya utoaji wa mikopo ya Sh600 milioni kwa vikundi 60 katika Manispaa ya Moshi, akieleza kuwa tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, Mkoa wa Kilimanjaro umetenga Sh9 bilioni kwa ajili ya mikopo hiyo, huku Manispaa ya Moshi ikiongoza kwa kutoa Sh5.9 bilioni kwa vikundi 758. Amesema pamoja na mafanikio yaliyopatikana, bado changamoto kubwa ni urejeshaji wa mikopo, ambapo zaidi ya Sh900 milioni bado hazijarejeshwa na baadhi ya vikundi, hali inayowanyima fursa wananchi wengine waliokuwa wakisubiri kunufaika na mikopo hiyo. Kutokana na hali hiyo, ameagiza fedha zote zinazodaiwa kurejeshwa haraka na kutolewa kwa taarifa ya marejesho kila baada ya wiki mbili. Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, amesema baadhi ya wanufaika hushindwa kurejesha mikopo kutokana na kubadili miradi baada ya kupokea fedha, tofauti na waliyoainisha wakati wa kuomba mkopo, jambo linalosababisha biashara kushindwa kuleta faida iliyotarajiwa. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa mikopo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi, Mwajuma Nasombe, amesema tangu kufunguliwa kwa dirisha la awamu ya sita Novemba 2024, Manispaa imetoa mikopo ya Sh2.7 bilioni kwa vikundi 281, ambapo Sh1.35 bilioni zimetolewa kwa vikundi vya wanawake, Sh1.32 bilioni kwa vijana na Sh49.7 milioni kwa vikundi vya watu wenye ulemavu.