У нас вы можете посмотреть бесплатно Mkuu wa wilaya aingilia kati mgomo wa madereva Daladala Himo или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Moshi. Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, amelazimika kuingilia kati mgogoro wa madereva daladala na bajaji katika eneo la Njia Panda, Mji mdogo wa Himo, baada ya madereva daladala kugoma kwa zaidi ya saa tano wakilalamikia kunyimwa abiria kwenye vituo vyao. Mgomo huo umetokea leo Februari 25, 2026, ukihusisha madereva daladala wanaofanya safari za Moshi–Marangu, wakidai kuwa madereva bajaji wamekuwa wakipakia na kushusha abiria katika vituo vyao vilivyopo kandokando ya barabara ya Marangu–Mwika, hali iliyosababisha mvutano na kusimamisha huduma ya usafiri kwa muda. Akizungumza eneo la tukio, DC Mnzava aliagiza madereva bajaji kuondoka mara moja katika eneo hilo na kurejea katika kituo chao cha awali cha Bavaria walichopangiwa na mamlaka husika, akisema hatua hiyo inalenga kuondoa mwingiliano na kurejesha utulivu wakati suluhu ya kudumu ikitafutwa. Aidha, aliwataka madereva daladala kusitisha mgomo huo na kuendelea na kazi ya kutoa huduma kwa wananchi ili kuepusha usumbufu wa usafiri, huku akisisitiza kuwa Serikali haitavumilia vitendo vinavyoweza kuvuruga amani na utaratibu wa usafirishaji. Kwa upande wao, Katibu wa Umoja wa Madereva Moshi–Marangu, Venance Minja, alisema bajaji zimekuwa kikwazo kwa biashara yao kutokana na kuingilia vituo rasmi vya daladala, wakati mwakilishi wa madereva bajaji Himo, Peter Mjema, akidai wao wamekuwa wakinyanyaswa na wenzao na kwamba eneo la Bavaria walilopangiwa si rafiki kwa shughuli zao za kila siku.