У нас вы можете посмотреть бесплатно Aliyefariki na kuzikwa akutwa hai, Polisi yaanza uchunguzi, Baba mzazi asimulia или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
"Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firaun" ndiyo kauli unayoweza kuitumia kuelezea tukio la Mtoto, Mabirika Wilson (8) ambaye anadaiwa kufariki na kuzikwa nyumbani kwao katika kijiji cha Salong'we kata ya Mwamabanza wilayani Magu mkoani Mwanza kisha siku 10 baadae akakutwa akiwa hai katika kijiji cha Mwangika wilayani Kwimba mkoani hapa. Mtoto huyo anayedaiwa kufariki kwa ugonjwa wa malaria Aprili 16 mwaka huu na kuzikwa siku moja baadae Aprili 17,2023 alikutwa na wachugaji wa ng'ombe akizurura kwenye majaruba yaliyoko kijiji cha Mwangika wilayani Kwimba mkoani Mwanza. Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Wilbroad Mutafungwa wafugaji hao baada ya kubaini kuwa mtoto huyo hana uangalizi walimuhoji akajitambulisha kuwa anaitwa Mabirika Wilson na nyumbani kwao ni kijiji cha Salong'we kilichopo wilaya ya Magu.