У нас вы можете посмотреть бесплатно TAKUKURU YAWAASA WATENDAJI KUZINGATIA THAMANI YA FEDHA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Moshi. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imewaasa watendaji wa Serikali wanaosimamia miradi ya maendeleo, hususan sekta ya afya, kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa kuzingatia thamani halisi ya fedha za umma ili kuleta manufaa kwa wananchi. Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila, amesema taasisi hiyo haitasita kuchukua hatua kali dhidi ya watendaji wazembe au wanaokwaza utekelezaji wa miradi kwa makusudi, akisisitiza kuwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za matumizi ya fedha za umma atachukuliwa hatua za kisheria. Chalamila aliyasema hayo wakati akikabidhi mashine ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi, akiwataka watumishi wa sekta ya afya kuitunza vifaa tiba hivyo pamoja na miradi mingine inayotekelezwa na Serikali. Daktari Bingwa wa Watoto hospitalini hapo, Dk Jonas Kessy, amesema hospitali inapokea idadi kubwa ya watoto njiti, hivyo mashine hiyo itasaidia kuimarisha huduma za uangalizi na kuongeza nafasi ya watoto hao kuishi. Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk Abillah Issa, amesema ujio wa mashine hiyo ni hatua muhimu katika kuboresha huduma za afya kwa watoto wachanga na kupunguza changamoto zinazowakabili wahudumu wa afya.