У нас вы можете посмотреть бесплатно TAG GEITA PENUEL CHRISTIAN TABERNACLE IBADA YA JUMAPILI 08/03/2026 REV ANNAEL G. PALLANGYO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
TAG GEITA PENUEL CHRISTIAN TABERNACLE IBADA YA JUMAPILI 08/03/2026 :REV ANNAEL GOTTLOB PALLANGYO 0755858880 SOMO: COMMITMENT/ KUJITOA KIKAMILIFU Luk.9:21-26;Esta.4:15-16; Mt.11:12,28-29 Kiini: if you are not commited I am not responsible; (kama hujajitoa na kujikabidhi kikamilifu mimi siwajibiki) Are You? Utangulizi Neno hutenda kazi pale mtu anapojikabidhi kwa aliyelisema tu. Ukristo wa kweli haujengwi juu ya urahisi, bali juu ya kujitoa kabisa kwa Mungu. Watu wengi wanataka: • Wokovu bila kubadilika • Baraka bila kujitoa • Mbingu bila kubeba msalaba Lakini katika andiko hili Yesu Kristo anaweka wazi kuwa kumfuata Yeye kuna gharama. Ukristo wa kweli hauko kwenye: • kuimba na kurukaruka • kusikiliza mahubiri na kuyaacha • au kwenda kanisani na ku-enjoy Ukristo wa kweli ni maisha ya kujitoa kabisa kwa Kristo. (Commitment) 1. Commitment ni neno linalomaanisha kujitolea kikamilifu na kujikabidhi, kwa jambo au kusudi fulani kwa uaminifu, uwajibikaji na uthabiti hadi litimie. Ni hali ya mtu kuamua moyoni na akilini kwamba hatarudi nyuma hata kama kuna changamoto. Maana Rahisi Commitment ni Uamuzi thabiti wa kusimama na kutekeleza jambo hadi likamilike. Vipengele vya Commitment/Kujitoa huku. • Uamuzi wa ndani (Inner decision) – mtu anaweka azimio moyoni. • Uaminifu (Faithfulness) – • kusimamia ahadi au wajibu bila kuyumba. • Uvumilivu (Perseverance) – kuendelea hata wakati kuna ugumu. • Uwajaibikaji (Responsibility) – kuchukua jukumu la matokeo ya kile ulichoamua. Mifano Rahisi na ya kawaida: • Mwanafunzi anayesoma kila siku hadi amalize masomo yake anaonyesha commitment kwa elimu yake. • Mtu anayefanya kazi kwa bidii ili kutimiza kusudi lake ana commitment kwa malengo yake. Katika Muktadha wa Kiroho • Commitment ni kujitolea kwa • Mungu na kusudi lake bila kurudi nyuma. Yoshua 24:15 "Mimi na nyumba yangu tutamtumikia Bwana." Dan.3:17-18 "hata asipotuokoa hatutaitumikia miungu yako ee mfalme" Hii inaonyesha uamuzi wa kudumu wa kumtumikia Mungu. Note: Commitment ni daraja kati ya kusudi na mafanikio. Bila commitment, hata uwe na maono makubwa hayawezi kutimia. ✔️ Maono + Commitment = Matokeo 1. Ngazi 3 za Commitment Kuna madaraja ya kujitoa na kujikabidhi, hebu tuone hapa: 1. Kujitoa na kujikabidhi kwa Maneno (Verbal Commitment) Hii ni ngazi ya kwanza ambapo mtu anasema ana nia, lakini hajathibitisha kwa matendo. Dalili zake • Anaahidi sana • Anazungumza vizuri • Anaonyesha hamasa ya muda mfupi Tatizo lake Maneno bila matendo hayazai matokeo. Mfano wa Biblia Mathayo 21:28–30 Mwana wa kwanza alisema: "Sitaenda." Lakini baadaye akaenda. Mwana wa pili alisema: "Nitaenda." Lakini hakuenda. 👉 Huyu wa pili alikuwa na commitment ya maneno tu. Funzo Watu wengi wako kwenye ngazi hii: wanaahidi kumtumikia Mungu wanaahidi kubadilika lakini hawatekelezi. 2. Commitment ya Matendo (Active Commitment) Hapa mtu anaanza kufanya kitu, si kusema tu. Yuko hivi: • anahudhuria kila kusanyiko • anajifunza kila siku • anafanya kazi kwa bidii • anashiriki kila jambo na wengine. • Hakatishwi tamaa wala • kuvunjwa moyo. Mfano: Luka 9:59-62 “Mtu yeyote akishika jembe kisha akatazama nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.” Hii inaonyesha commitment ya kweli inaonekana kwenye vitendo. Mfano: Mitume wa Yesu: Mathayo 4:20 “Mara wakaziacha nyavu zao wakamfuata.” Walionyesha commitment kwa kuacha kazi zao. Umeacha nini? 3. Commitment ya Moyo na Maisha (Total Commitment) Hii ndiyo ngazi ya juu kabisa. Mtu anajitoa: • moyo • muda • nguvu • maisha yake yote. Hakuna kurudi nyuma. Mfano: Danieli 3:16–18 Shadraka, Meshaki na Abednego walisema: “Mungu wetu anaweza kutuokoa… lakini hata asipotuokoa, hatutaitumikia sanamu yako.” Hii ni commitment ya maisha yote. Mfano mwingine Mtume Paulo Wafilipi 1:21 “Kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida.”