У нас вы можете посмотреть бесплатно DC TANGANYIKA AKAGUA MIUNDOMBINU KAKOSO SEC ATOA MAELEKEZO KUIMARISHA MAHUDHURIO MAANDALIZI YA FORM5 или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
DC TANGANYIKA AKAGUA MIUNDOMBINU SHULE YA SEKONDARI KAKOSO, ATOA MAELEKEZO KUIMARISHA MAHUDHURIO NA MAANDALIZI YA KIDATO CHA TANO Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Mhe. Onesmo Buswelu, ametembelea Shule ya Sekondari Kakoso iliyopo Kata ya Tongwe, Wilaya ya Tanganyika, kwa lengo la kukagua hali ya shule, mahudhurio ya wanafunzi, maendeleo ya miundombinu na maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaotarajiwa kuanza masomo shuleni hapo. Katika ziara hiyo, Mhe. Buswelu amezungumza na walimu kuhusu hali ya mahudhurio na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya walimu, wazazi na viongozi wa Serikali katika kuhakikisha wanafunzi wanaripoti na kuhudhuria masomo kwa wakati, ili kuongeza ufaulu na kuimarisha nidhamu shuleni. Aidha, amekagua ujenzi wa matundu manne (4) ya vyoo vya wasichana pamoja na bweni la wanafunzi, na kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, Bw. Shabani J. Juma, kuhakikisha miundombinu ya maji na umeme inakuwa katika hali ya kufanya kazi kikamilifu. Vilevile, amewaagiza wasimamizi wa ujenzi wa bweni kuhakikisha wanamtafuta fundi aliyeshiriki ujenzi ili kukamilisha mifumo ya umeme ndani ya bweni hilo. Sambamba na hilo, Mhe. Buswelu amemuagiza Mkuu wa Shule kuunda Kamati ya Mazingira na Afya ya Shule itakayoratibu masuala ya usafi, afya na mazingira, pamoja na kuhamasisha wazazi kujiandikisha katika Mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote ili wanafunzi wapate huduma za afya kwa urahisi. Pia amemuagiza Mtendaji wa Kata ya Tongwe, Bw. Cleophas J. Ngwenga, kwa kushirikiana na Afisa Elimu Kata na watendaji wengine, kuunda timu ya ufuatiliaji wa wanafunzi ambao bado hawajaripoti shuleni, huku akisisitiza hatua za kisheria kuchukuliwa kwa wazazi au walezi watakaobainika kuchangia utoro bila sababu za msingi.