У нас вы можете посмотреть бесплатно MAMA MAKINDA: MZEE MSUYA ALIKUWA JIRANI YANGU, KWAKE KULIKUWA HAKUNA MFANYAKAZI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anne Makinda, amesema Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, hayati Cleopa David Msuya, ni mfano wa kugwa kwa namna alivyoishi maisha ya upendo, nidhamu na mfano wa kuigwa kwa viongozi wa sasa. Akizungumza wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa Msuya leo, Jumapili, Mei 11, 2025, jijini Dar es Salaam, Makinda amesema aliwahi kuwa jirani na familia ya Msuya maeneo ya Seaview, na alishuhudia kwa karibu namna kiongozi huyo na mkewe, marehemu Rhoda Mshana, walivyoishi maisha ya utu na usafi wa maadili. "Ukifika nyumbani kwao utawa-admire (utawatamani). Mkewe alikuwa msafi sana, mwenye nidhamu, na maisha yao yalikuwa ya mfano wa kuigwa. Walikuwa wanapenda watu na kuishi nao kwa upendo mkubwa, maisha ya Msuya ni funzo kwa viongozi wa sasa kuhusu namna ya kuishi kwa heshima, utu na kuwajali wengine," amesema Makinda. Cleopa Msuya alifariki dunia Jumatano, Mei 7, 2025, katika Hospitali ya Mzena, Kijitonyama jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya moyo. Mwili wake umeagwa leo kwa heshima ya kitaifa, na unatarajiwa kuzikwa keshokutwa Jumanne, Mei 13, 2025, katika kijiji chao cha Usangi, wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro. Video na Ally Mlanzi