У нас вы можете посмотреть бесплатно WAVAMIA MAKABURI NA KUIBA MISALABA MOROGORO или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Watu wasiofahamika wamevunja na kuondoka na misalaba iliyowekwa kwenye makaburi ya Kola, mkoani Morogoro. Hatua hiyo imesababisha ndugu wa marehemu waliozikwa kwenye makaburi hayo kushindwa kuyatambua, huku wengine wakiingia hasara ya kuweka misalaba mingine. Hii ni mara ya pili kutokea kwa matukio hayo ya kuvunjwa na kuibwa kwa misalaba na baadhi ya watu wanadai wanaoiba misalaba hiyo wanakwenda kuuza kama chuma chakavu. Mwananchi limefika katika makaburi hayo na kujionea uharibifu huo uliofanywa na watu hao. Ramadhani Libenanga, ndugu wa marehemu aliyefika makaburini hapo amesema ameshuhudia makaburi matatu ya ndugu zake yakiwa wameibwa misalaba na makaburi mengine zaidi ya 50 nayo yakiwa hayana misalaba. Mkurugenzi wa Manispa ya Morogoro, Emanuel Mkongo amesema taarifa za wizi wa misalaba amezipata kupitia kwa wataalamu wake na tayari ameshaanza kuzifuatilia kwa karibu, ikiwa ni pamoja na kutafuta njia ya kudhibiti wizi huo. Soma zaidi kwenye tovuti ya Mwananchi. VIDEO NA HAPPYNES MREMI