У нас вы можете посмотреть бесплатно VVU NA UNYONYESHAJI/WIKI YA UNYONYESHAJI IRINGA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Wiki hii ni wiki ya maadhimisho ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama Duniani maadhimisho ambayo kila Mwaka hufanyika kila mwaka tarehe 1-7 Julai. Nchini Tanzania mkoa wa Iringa unaungana na wengine hapa Nchini kuadhimisha wiki hii ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama, lengo la siku hii ni kulinda , kuimarisha na kuendeleza unyonyeshaji wa maziwa ya mama. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Queen Sendiga anasema Iringa inashika nafasi ya tatu kitaifa kwa tatizo la watoto wenye udumavu kwa asilimia 47.1 ikiongozwa na Mkoa wa Njombe sambamba na hilo anasema kuwa ni asilimia 66 ya watoto mkoani humo wananyonya maziwa ya mama pekee miezi 6 ya mwanzo. Unyonyeshaji na VVU, Hatuwezi kuzungumzia wiki hii ya unyonyeshaji pasipo kulizungumzia kundi maalum la wakina mama wanaoishi na maambukizi ya VVU, je wao wanafanya nini katika kumlinda mtoto na kuhakikisha ananyonya miezi sita mfululizo? Ni katika Mkoa wa Iringa mama ambaye hajataka jina lake kujulikana, mtoto wake ana umri wa chini ya miezi sita, anasema awali tangu kuzaliwa kwake hakuwahi kujua kama ameathirika mpaka alipougua sana ndipo mama yake akamfahamisha kwamba alizaliwa na maambuizi ya VVU, maisha yakaendelea kwa kuanza kutumia dawa, ” nilipata mchumba wa kwanza tulipoenda kupima alipojua nimeathirika akaniacha, anasema mama huyu, ndipo nilipata mwingine baadae na kuzaa naye mtoto, nilijifungua salama salmini na mtoto wangu ni mwenye afya kama mnavyo muona na sasa nasubiri kipimo kujua kama hakupata maambukizi au la…..” Wahudumu wa afya ngazi ya jamii ndio wafuatiliaji wa afya kwenye kaya, Janerose Nyeho ni msimamizi wa wahudumu hao kutoka kituo cha Alamano Lakini pia zipo changamoto Zipo tofauti za unyonyeshaji kwa mtoto ambaye yuko kwenye hatari ya kuambukizwa, na mtoto ambaye amegundulika ana maambukizi, sambamba na hilo itokeapo mama ambaye ana maambukizi amepata michubuko kwenye matiti yake nini anapaswa kufanya bila kusahau lini mama huyu aache kunyonyesha? kutoka kituo cha afya cha Ngome Muuguzi kitengo cha afya ya mama na mtoto Yusta Materu anasema Mwisho Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mafunzo na Elimu ya Lishe kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Esther Nkuba anasema serikali imeweka mikakati madhubuti kwa kutenga bajeti kwa watoa huduma ngazi ya jamii na huku akisisitiza wamama kuendelea kunyonyesha huku wakijikinga na UVIKO 19. KAULI MBIU 2021 “KULINDA UNYONYESHAJI WA MAZIWA YA MAMA NI JUKUMU LETU SOTE” Kutoka Iringa Mimi ni Tukuswiga Mwaisumbe. #wizarayaafyajiniawanawakenawatoto #globalvolunteer #rcpprogram #taasisiyachakulanalishe #lisheendelevu #childrenincrossfare@watotowetutunuyetu