У нас вы можете посмотреть бесплатно DC LUDEWA ATATUA MGOGORO WA ARDHI KIJIJI CHA MADUNDA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Ikiwa ni muendelezo wa ziara yakupita Kijiji kwa Kijiji kwa lengo la kutatua kero za wananchi na kufanya mikutano ya hadhara Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Olivanus Thomas amefanya ziara katika Kijiji cha Luana kilichopo katika kata ya Luana na Kijiji cha Madunda kata ya Mawengi. Katika ziara hiyo mkuu wa Wilaya huyo ameambatana na Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo ndugu Castor Kibasa, baadhi ya wakuu wa idara pamoja na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri hiyo. Akiwa katika kikao alichokifanya na viongozi wa serikali ya Kijiji chaLuana mkuu huyo aliwataka viongozi wa Kijiji hicho kuhakikisha wanasimamia vizuri swala la ulinzi na usalama kwa wananchi ili wananchi waweze kuishi kwa amani. Aidha katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya amefanikiwa kusuluhisha mgogoro wa ardhi kati ya Kanisa Katoliki Parokia ya Madunda na familia ya Alloyce Willa uliohusisha shamba la miti la hekari tano. Pia mkuu huyo alitamatisha ziara yake kwa kufanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Madunda kata ya Mawengi kwa kusikiliza kero na changamoto mbalimbali na wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.