У нас вы можете посмотреть бесплатно Hatari! Dawa za ARV zinavyotumika kunenepesha mifugo, madhara kwa binadamu yatajwa или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Matumizi ya dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARV) kunenepesha mifugo, yametajwa kushika kasi nchini na kuchangia usugu wa dawa hizo unaotokana na ulaji wa mazao ya mifugo kama vile kuku na nguruwe. Kutokana na hilo, Serikali imelazimika kufanya vikao na wadau wa sekta ya afya na mifugo kuweka mikakati ya pamoja kutafuta suluhisho la udhibiti wa matumizi holela ya dawa na kutoa elimu kwa jamii. Mratibu wa Afya Moja kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Dk Mololo Noah amesema hayo leo Septemba 20, 2024 kwenye kongamano lililokutanisha wadau wa afya, mifugo, watafiti, na wanasayansi kutoka vyuo mbalimbali kujadili changamoto za sekta ya afya lililoandaliwa na Shirika la HJFMRI. "Kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi holela ya ARV kunenepesha kuku na nguruwe hali inayochangia mlaji kupata madhara ya usugu wa dawa kutokana na wingi wa mabaki ya vimelea kwenye kitoweo," amesema. Hata hivyo, amesema bado hawana takwimu kwa sababu wanandelea kufanya utafiti na sasa wako kwenye kampeni ya mkoa kwa mkoa ambayo wakiimaliza watakuwa na uhalisia wa picha kamili na kutoa taarifa. Dk Noah amesema kutokana na changamoto hiyo, sekta ya afya inaendelea na udhibiti na kutoa elimu kwa wananchi kuachana na matumizi yasiyo sahihi.