У нас вы можете посмотреть бесплатно WAMAREKANI WAFURIKA MITAANI KUMPINGA TRUMP, ELON MUSK, SABABU NI…. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Washington. Maelfu ya raia wa Marekani kutoka maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wamefurika mitaani katika kile ambacho kinatajwa kuwa ni kupinga mwenendo wa utendaji kazi wa sasa wa Rais wa taifa hilo, Donald Trump na swahiba wake, Elon Musk ambaye amekuwa akiongeza machungu kwa kupunguza matumizi ya Serikali. Kutokana na mwenendo huo wa Serikali ya Trump, jamii ya Wamarekani wengi wamejikuta wakipitia wakati mgumu kutokana na baadhi yao kufutwa kazi katika kile kinachotajwa ni kuongeza ufanisi wa Sekta za Umma. Uamuzi huo ulianza kutekelezwa baada Rais Donald Trump kuapishwa kuingia Ikulu ya White House, Januari 20, mwaka huu akirithi mikoba kutoka kwa Rais Joe Biden wa Democrats. Shirika la Habari la Associated Press limeripoti leo Jumapili Aprili 6,2025, kuwa maandamano hayo yaliyoitwa Hands Off! yaliandaliwa katika zaidi ya maeneo 1,200 katika majimbo yote 50, yakihusisha zaidi ya makundi 150, yakiwemo mashirika ya haki za kiraia, vyama vya wafanyakazi, watetezi wa jamii ya wapenzi wa jinsia moja, mashujaa wa vita na wanaharakati wa uchaguzi. Video na Mgongo Kaitira.