У нас вы можете посмотреть бесплатно #BMGTV или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Mwaka 2018 ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu katika Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza yenye urefu wa kilomita 9.7 uligharimu shilingi bilioni 18 ukijumuisha barabara nyingine ambazo ni Isamilo-Big Bite hadi Mji Mwema kilomita 1.2 na Makongoro Junction-Mwaloni mpaka Kigoto Kirumba kilomita 1.2 ukitekelezwa na kampuni ya Sinohydro Corporation LTD. Pia mwaka 2016 zaidi ya bilioni mbili zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya sherehe za Muungano zilibadilishwa matumizi na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Magufuli na kuelekeza zitumike kwenye upanuzi wa barabara ya Makongoro-Airport kutoa njia mbili hadi njia nne kuanzia eneo la Ghana Quarter hadi uwanja wa ndege wa Mwanza. Fuatilia mwonekano wa kazi iliyofanyika katika barabara hizo kuanzia eneo la Buswelu-Sabasaba ambapo tamati itakuwa mzunguko wa barabara ya Kenyatta/ Rock City. BMG Online Media- Pamoja Daima! Tovuti https://www.bmgblog.co.tz/ Facebook / bmghabari Twitter / bmghabari Instagram / bmghabari #BMGTV #BMGBLOG #BMGHABARI #PamojaDaimaBMG