У нас вы можете посмотреть бесплатно WANANCHI WAASWA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA MASHUJAA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
WANANCHI RUVUMA WAASWA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 120 YA MASHUJAA. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Hamad Hassan Chande, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya miaka 120 ya mashujaa wa Vita ya Majimaji yatakayofanyika Februari 27. Wito huo umetolewa wakati alipotembelea na kukagua maandalizi ya maadhimisho hayo katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa ya Vita ya Majimaji mjini Songea. Amesema wananchi wanapaswa kushiriki ili kujionea kumbukumbu mbalimbali na kupata historia ya namna mashujaa wa Majimaji walivyopambana kwa ujasiri hadi kufanikisha kupatikana kwa uhuru wa taifa. Aidha, Mhe. Chande amesisitiza kuwa wilaya na mikoa yenye makumbusho kama hayo yahakikishe yanatunzwa na kuenziwa, huku akibainisha kuwa serikali ipo tayari kushirikiana na wadau kufufua upya historia hiyo na kuitangaza duniani. Ameongeza kuwa nchi nyingi hujipatia mapato kupitia makumbusho ya kihistoria, hivyo ni wajibu wa Watanzania kuyathamini na kuyatumia kama nyenzo ya kukuza uchumi na kuendeleza urithi wa taifa.