У нас вы можете посмотреть бесплатно MJUE ELIAS KIHOMBO A-Z T.O BORA WA MUDA WOTE TANZANIA, ALIKUWA NA AKILI BALAA,SAYANSI ILIKUA KICHWAN или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#EliasKihombo #physics #HistoriayaTowa2006EliasKihombo Alishika namba 1 kitaifa matokeo ya mitihani Kidato cha sita mwaka 2006, Elias Kihombo pichani aliyesoma PCM alipata division 1.3 akiwa na A za juu katika masomo yote kuliko wanafunzi wengine wote wa michepuo mingine kitaifa. Alihitimu secondary ya Tosamaganga Kidato cha nne pia alihitimu Tosamaganga 2003, inaelezwa alipata division 1.14 akiwa na alama A katika Physics na Chemistry pamoja na B katika Mathematics na Biology, hivyo matokeo yake Kidato cha nne japo alifanya vizuri lakini wengi hawakumtarajia sana kama angekuja kushika nafasi ya Kwanza kitaifa form 6 kwa kupata alama za juu zaidi Baada ya form six alijiunga na University Of Dar es salaam(UDSM) alichukua BSc In Telecommunication Engineering(4yrs) lakini ikiwa imebaki miezi michache kabla hajahitimu inaelezwa ali-disco katika hali ambayo imewaacha wengi na maswali vichwani Hata hivyo, mitandaoni wengi waliosoma michepuo ya PCM na PCB wanamsifu sana Elias Kihombo kwamba alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufundisha hasa Physics hata maswali magumu yaliyo watatiza wengi bila yeye kushika kitabu. Ali-solve maswali Kwa njia wanayojua wengi kisha wanasema alikuwa akitumia njia nyingine kama tano wasizozijua au za kwake halafu jibu linakuja lilelile Elias Kihombo alizunguka katika shule nyingi kongwe na maarufu za secondary zenye wanafunzi wanaotajwa kuwa na vipaji maalum aliwasaidia, alijaza watu wengi sana katika tuitions zake wanafunzi waliambiana akija wasikose kwenda. Imeeleza hata kabla hajahitimu degree yake ya kwanza tayari alitunga vitabu vyake vya Physics ambavyo viliuzika sana Baada ya ku-disco UDSM, inaelezwa takribani miaka nane baadaye alirudi tena kuanza upya kusoma BSc In Petroleum Engineering ila kabla ya kuhitimu alifar!ki dunia 2020 Kwa siku kadhaa sasa, mitandaoni Elias Kihombo posts kumhusu zinasambaa sana wengi waliopitia mikononi mwake katika somo la Physics wakimtaja kwamba bila shaka yeye ndie Tanzania One maarufu zaidi na genius zaidi kuwahi kutokea Bongo. Inaelezwa shule nyingi za secondary zilitaka kumpa ajira ya kudumu kufundisha ila alikataa ili kufanya ziara zake za kufundisha tuition shule mbalimbali nchini Nini mtazamo wako, kuna T.O mwingine mkali zaidi kumzidi Elias Kihombo? Kwa undani Zaidi tumekuwekea video nzima hapa MABENA TV Subscribe upate mengi Zaidi