У нас вы можете посмотреть бесплатно MAJERUHI WAZUNGUMZA JINSI AJALI ILIVYOTOKEA PALE MBEMBELA MBEYA или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Idadi ya watu waliofariki kwenye ajali ya barabarani iliyotokea jana Juni 5,2024 eneo Mbembela Jijini Mbeya imeongezeka kutoka watu 13 na kufikia 15. Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Dkt.Godlove Mbwanji akizungumza na waandishi wa habari amesema jana walipokea jumla ya wahanga 34 , kati ya hao waliofariki walikuwa 13 na majeruhi 21 kati ya hao majeruhi 21 wawili wamefariki na ongeza idadi ya waliofariki na kufikia 15 na majeruhi kubakia 19 kati ya hao majeruhi sita (6) waliruhusiwa baada ya kupatiwa matibabu na kufanya idadi ya majeruhi wanaondelea kupata matibabu hospitalini hapo kuwa 13, wanaume 10 na wanawake watatu (3). Dkt.Mbwanji ameongeza kuwa kati ya watu 15 waliofariki, 10 ni wanaume na watano (5) ni wanawake na mpaka sasa miili ya watu wanne (4) waliofariki katika ajali hiyo, bado haijatambuliwa na majeruhi 15 wamelazwa wakiendelea na matibabu, kati yao majeruhi watatu wamelazwa kwenye chumba cha uangalizi maalum(ICU). Mkurugenzi huyo wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, amefafanua kuwa mgonjwa mmoja mwanaume ambaye amelazwa kwenye wodi ya kawaida bado ndugu zake hawajajitokeza kwakuwa alipata mtikisiko kichwani na anashindwa kujieleza ingawa hali yake inazidi kuimarika pia mwanamke aliyelazwa chumba cha uangalizi maalum(ICU) pia hajatambuliwa na ndugu zake.