У нас вы можете посмотреть бесплатно EPISODE 32 : TUNDU LISSU APINGA USHAHIDI WA MAUAJI YA OKTOBA 29 KUINGIZWA KWENYE KESI YA UHAINI или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Updates: Kesi ya Uhaini Inayomkabili Tundu Lissu (Februari 23, 2026) Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, inatarajiwa kutoa uamuzi wa kama ni sahihi au la kupokelewa kwa notisi ya ushahidi wa ziada kwenye ushahidi wa shahidi wa 26 katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu. Hoja za Upande wa Jamhuri Shauri hilo linasikilizwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru. Mapema leo, upande wa Jamhuri kupitia kwa Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, uliieleza mahakama kuwa unataka kuwasilisha notisi ya ushahidi wa ziada wa shahidi ambaye ni Askari Mpelelezi, ACP Amini Mahamba. Wakili Katuga alibainisha yafuatayo: Mnamo Februari 18, 2026, waliwasilisha (file) notisi ya kuongeza ushahidi kwa njia ya mtandao kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (sura ya 20, mapitio ya 2023). Ushahidi huo ni wa nyongeza kwa shahidi ACP Amini Mahamba, ambaye hakuwekwa na kusomwa wakati wa shauri la mwenendo kabidhi (committal proceedings). ACP Amini Mahamba ndiye aliyekuwa kiongozi wa timu ya upelelezi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, na kile alichokipata ndicho kilichopo kwenye kiini cha nyongeza hiyo. Pingamizi la Tundu Lissu Mshitakiwa, Tundu Lissu, ameweka pingamizi dhidi ya kupokelewa kwa ushahidi huo akitoa hoja zifuatazo: Kisheria: Kwa mujibu wa kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinachopaswa kupokelewa ni maelezo ya shahidi ambaye hakuwepo wakati wa mahakama ya ukabidhi, na si kuongeza ushahidi wa shahidi ambaye tayari alishatoa ushahidi wake. Muda wa Matukio: Lissu ameeleza kuwa si sahihi kupokea ushahidi huo kwani unazungumzia matukio ya Oktoba 29 na kuendelea, wakati yeye makosa anayoshtakiwa nayo yalitokea Aprili 3, 2025. Hali ya Kizuizini: Alikamatwa Aprili 9 na kushtakiwa Aprili 10, 2025, na tangu wakati huo amekuwa akishikiliwa gerezani. “Nipo tayari kujadili ya Oktoba 29, watayaweza? Oktoba kulikuwa kuna mauaji ya halaiki na ni magumu,” alisema Lissu. Endelea kufuatilia Uhuru Online Media kwa updates zaidi za shauri hili mwanzo hadi mwisho. #tundulissu #mahakamani #chadema