У нас вы можете посмотреть бесплатно WAWILI KORTINI KWA TUHUMA ZA WIZI WA BIL. 1 ZA NSSF или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
#HABARI: Watu wawili, akiwemo mmiliki wa Kampuni ya Salaaman Health Services Ltd, Abdi Hirsi, na Afisa Rasilimali Watu, Elia Makongwa, wamefikishwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza wakikabiliwa na mashtaka 841 ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha. Washtakiwa hao wanatuhumiwa kuisababishia Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) hasara ya zaidi ya shilingi bilioni moja kati ya mwaka 2021 na 2023 kupitia genge la uhalifu lililofanya kazi mkoani Mwanza na Dar es Salaam. Upande wa Jamhuri umeeleza kuwa washtakiwa walighushi nyaraka za wagonjwa na kuzitumia kujipatia fedha isivyo halali kutoka ofisi za NSSF jijini Dar es Salaam, wakidai kutoa huduma za matibabu katika kituo chao cha Salaaman mkoani Mwanza. Mashtaka hayo yanajumuisha kuongoza genge la uhalifu, kughushi, na kutumia nyaraka za uongo, ambapo wanadaiwa kupokea shilingi bilioni 1.011 huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao la uhalifu. Hakimu Mfawidhi Erick Maley ameahirisha kesi hiyo namba 2330 ya mwaka 2026 hadi Februari 24 baada ya kutoa uamuzi mdogo kuhusu ombi la matibabu kwa mshtakiwa wa kwanza, akielekeza mamlaka za magereza kumpatia huduma ya afya kwa mujibu wa taratibu. Washtakiwa wamerudishwa rumande huku upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Fadhiri Mwandolomo ukiendelea na taratibu za kisheria. Powered by #MCHEZOSUPA JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA: - Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M - Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV. #ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania #Follow @itvtz @radioonetanzania @capitaldigitaltanzania Usisahau kutufuatilia katika mitandao yetu ; Subscribe to our Youtube Channel : http://bit.ly/itvtanzania Facebook : https://bit.ly/2KeQNl3 Twitter : https://bit.ly/2XG7aii Instagram : https://bit.ly/34KItmg