У нас вы можете посмотреть бесплатно RAIS SAMIA AMLILIA MTOTO ALBINO ALIYEUAWA KIKATILI. или скачать в максимальном доступном качестве, видео которое было загружено на ютуб. Для загрузки выберите вариант из формы ниже:
Если кнопки скачивания не
загрузились
НАЖМИТЕ ЗДЕСЬ или обновите страницу
Если возникают проблемы со скачиванием видео, пожалуйста напишите в поддержку по адресу внизу
страницы.
Спасибо за использование сервиса ClipSaver.ru
Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ameguswa na kifo cha Mtoto Albino Asimwe Novart mwenye umri wa miaka miwili na nusu ambaye ameuawa kwa kukatwakatwa viungo vyake katika eneo la Kamachumu lililopo Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera. Akiongea leo June 18,2024 wakati akishiriki Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari Jijini Dar es salaaam, Rais Samia amesema “Kuna kifo kimetokea na kimenigusa sana cha Mtoto mdogo alikuwa anacheza akatekwa wakamnyofoanyofoa, siku tatu hakijaonekana kimeonekana kimeharibika , tusimame kwa dakika moja tumuombee” Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera, Mtoto huyo alichukuliwa nyumbani kwao May 30 mwaka huu 2024 na mwili wake umepatikana jana June 17 na mpaka sasa Watu wanne wanashikiliwa kwa uchunguzi zaidi akiwemo Baba Mzazi wa Mtoto huyo. Mwili wa Mtoto huyo umekutwa umefungwa kwenye mfuko na kutelekezwa kwenye kalavati barabara ya Ruhanga-Makongora kata ya Ruhanga, Tarafa ya Kamachumu huku viungo vyake vikiwa vimekatwa.